Ruka kwenda maudhui kuu
MASHARTI YA HUDUMA

Masharti ya Huduma — MANE

Majuneo Group Limited • Kuanza: 04 Agosti 2026 • Toleo 1.0

Kwa kutumia MANE unakubali masharti haya. Tafadhali yasome. Kama hukubaliani, tafadhali usitumie huduma.

Wasiliana na DPO

1. Umiliki na Masharti

MANE ni program ya usimamizi wa kumbukumbu za kifedha (financial record-management software) inayomilikiwa na kuendeshwa na Majuneo Group Limited, Dar es Salaam, Tanzania. Programu hii imetengenezwa mahususi kwa vikundi vya VICOBA, Upatu na Chama — si benki, si pochi ya pesa, bali daftari la kidijitali linalosaidia kurekodi na kusimamia hesabu kwa uwazi.

Mmiliki: Majuneo Group Limited • Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania • Toleo 1.1 • 09 Septemba 2026

2. MANE si Benki — Dhima ya Kifedha

MANE ni mfumo wa kumbukumbu tu, si benki, si wallet ya pesa. Hatushiki, hatuhamishi, hatuoki pesa ya kikundi chenu. Pesa inabaki sandukuni / benki / simu ya kikundi kama ilivyo. Sisi tunarekodi tu kile mlichokifanya. Ada tunayopokea ni ya mfumo pekee (subscription).

⚠️ Kama kuna mtu anayekuomba utume pesa ya kikundi kwenda namba ya MANE — ni utapeli. Ripoti mara moja: +255 660 888 297.

3. Jaribio la Siku 30 na Usajili

Kila kikundi kipya kinapata jaribio huru la siku 30 (hadi wanachama 15) bila malipo yoyote. Katika kipindi hiki, mnaweza kutumia vipengele vyote — Hisa, Mikopo, Mfuko wa Jamii, Miradi na Ripoti — bila kikomo.

  • Baada ya siku 30, kuendelea kutumia MANE kunahitaji usajili hai wa kikundi kama ilivyoainishwa katika /bei. Bila usajili, hutaweza kuongeza miamala mipya — lakini data zote zinabaki salama na unaweza kuendelea kuiona.
  • Bei: Mini TSh 15,000, Kati TSh 20,000, Plus TSh 25,000, Max TSh 30,000 / mwezi — chagua kulingana na ukubwa wa kikundi. Angalia bei zote →
  • Bei yako imefungwa kwa miaka 2 tangu siku ya kuanza — tunaandika kwenye ankara yako. Hakuna kupanda ghafla.
  • Malipo kupitia Selcom Lipa Namba — uthibitisho wa HMAC na ulinganisho kila siku saa 3 asubuhi. VAT imejumuishwa. Hakuna ada ya siri.

💡 Ushauri: Anza na jaribio, kisha chagua kifurushi kinacholingana na idadi ya wanachama wenu kwa sasa — unaweza kubadilisha baadaye.

4. Ada na Malipo ya Kawaida (Selcom)

  • Kila mwaka okoa 15% ukilipia mwaka mzima.
  • Ukichelewa kulipa, data haifutwi — mnaendelea kuiona na kuipakua. Mkithubiria, mnarudi na data yote.

5. Dhima na Utawala wa Kikundi — Utaratibu wa Idhini ya Maafisa 3

Idhini ya mwisho ya utoaji wa mikopo, ugawaji wa faida (gawio), na uhamishaji wa fedha za mfuko inabaki mikononi mwa Maafisa 3 walioteuliwa wa kikundi — Mwenyekiti, Katibu na Mhazini — peke yao.

  • Kila ombi la mkopo, malipo ya faida, au uhamisho wa mfuko lazima lidhinishwe na Maafisa 3 wote ndani ya app. Hakuna afisa anayeweza kujidhinishia mwenyewe.
  • Mfumo unazuia kujikubali (self-approval) kiotomatiki — ukijaribu kujidhinishia, mfumo unakataa.
  • Kwa kutekeleza utaratibu huu, Majuneo Group Limited inaachiliwa dhidi ya wizi wa ndani wa kikundi, mianya ya maafisa, au migogoro ya ndani kuhusu fedha — jukumu la uaminifu na uamuzi wa mwisho ni la kikundi chenyewe.
  • Taarifa za uongo au wizi wa kumbukumbu — kikundi kinawajibika kisheria, na tunaweza kusitisha akaunti inayokiuka masharti.

⚖️ Muhimu: Majuneo Group Limited haisimamii pesa za kikundi, haidhinishi mikopo na haigawi faida — sisi ni watoa Programu tu. Uamuzi wote wa kifedha ni wa kikundi.

6. Majukumu ya Kikundi

  • Viongozi 3 ndio wanaowajibika kuandika na kuidhinisha kwa usahihi na kwa wakati.
  • Kila mwanachama ana haki ya kuona salio lake na historia yake — uwazi kwa wote.

7. Usalama & Kumbukumbu

Kila muamala una hash-chain HMAC-SHA256 na verification ya usiku (cron). Kumbukumbu ni za kikundi, si zetu. Mnapakua PDF/Excel wakati wowote. Data kuu huhifadhiwa offline-first na husawazishwa kwa HMAC-SHA256.

8. Kusitisha / Kufuta Akaunti

Mnaweza kughairi wakati wowote — hakuna mkataba wa muda mrefu. Data ya kibinafsi inafutwa ndani ya siku 30 baada ya ombi, isipokuwa miamala (ledger) inayobaki kwa miaka 5 kwa ajili ya ukaguzi. Tuna haki ya kusitisha akaunti inayokiuka masharti bila refund ya mwezi uliopo.

9. AI na Ushauri

AI coaching, tathmini ya riski na utabiri wa cashflow ni ushauri tu, si ushauri wa kisheria au wa uwekezaji. Maamuzi ya mikopo ni ya viongozi wa kikundi.

10. Sheria Inayotumika

Masharti haya yanasimamiwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Migogoro yoyote itakayojitokeza kutokana na matumizi ya MANE itatatuliwa kwanza kwa njia ya maridhiano, na ikishindikana, itapelekwa katika mahakama yenye mamlaka jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mahakama ya mwanzo: Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni / Ilala — Dar es Salaam. Lugha ya mkataba: Kiswahili na Kiingereza — Kiswahili kitatangulia endapo kuna utata.

11. Mawasiliano

Majuneo Group Limited, Mbezi Beach, Dar es Salaam, Tanzania
Email: info@majuneogroupltd.com • WhatsApp: +255 660 888 297
Tovuti: mane.co.tz • Toleo 1.1 • 09 Septemba 2026

Wasiliana nasi WhatsApp